KUFELI SHULE SIO KUFELI MAISHA

KUFELI SHULE SIO KUFELI MAISHA

Feb 09

Imenibidi niandike hii mada kutokana na watu ambao wanashadadia matokeo ya wenzao na kuyaandikia status kabisa haswa Facebook na Twitter…Hivi kwanini mtu unaanza tu kushabikia matokeo ya mwenzako tena mtu kama kafeli ndio unaandika kabisa Kiko wapi? mara blah blah?? Why is that?

Yani kama matokeo ya mtoto wa Rais wetu,Mwanaasha Jakaya Kikwete yamekuwa gumzo nchi zima utafkiri  huyo Mwanaasha sio binadamu kama binaadamu wengine..Kisa kapata division four..Haya hapo angepata One pia tungeeongea Ohh kapewa majibu!! Jamani kwanini Watanzania tunakua hivi?

 

Sitetei mtu kufeli ila jamani inatubidi tujue kuwa Kufeli nayo ni moja wapo ya hatua katika maisha…Wangapi wamefauli form 4,form 6 na leo wako wapi??? na wangapi hawajafika hata la saba lakini leo hii wanaonekana katika jamiii kuwa ni WATU?? Hebu tujifunze..

Na nafikiri kuwa kwa hawa wote wanaoshadadia wenzao kufeli labda hawajawi kufeli katika maisha yao, Ikikutokea utajua uchungu wa kufeli unaumaje na hata matokeo yakitoka unakua hauna mzuka nao Kwasababu unajua jinsi gani KUFELI inavyouma….I been there!

Cha msingi mpe moyo mtu  halafu kufeli shule sio Kufeli Maisha Jamani though Education is sexy and  Nasisitiza tena kuwa sitetei Kufeli ila atlist tujiweke kwenye viatu vya yule aliyefeli,ndio utajua namaanisha nini…

NI HAYO TU!

7 comments

  1. imomuns

    “kufeli shule sio Kufeli Maisha”.. ni kweli! na bila ya kufeli hatuwezi kujua mafanikio! ninsoza!!

  2. Anonymous

    wabongo wanachuki zao yule ni binadamu kama wengine wote na hao wanaomsema wasijifananishe nae yule atapelekwa zake nje ya nchi na atapiga kitabu akirudi hapa anamasters tayari wanaosema watabaki kupiga majungu mwenzao anasonga mbele.

  3. wabongo wanachuki zao yule ni binadamu kama wengine wote na hao wanaomsema wasijifananishe nae yule atapelekwa zake nje ya nchi na atapiga kitabu akirudi hapa anamasters tayari wanaosema watabaki kupiga majungu mwenzao anasonga mbele.

  4. Rogers Reventine

    Da bora ulivyowambia man kuna watu awana story zaid y kuwazngmzia wa2 waliofer asa pand fulan

  5. Kfeli n kfeli,
    &
    ku-pass n k-pass tu…
    *watu,
    wanaangalia shule ya mtu mliyosoma..
    Ndiyo waweza sema kitu..
    Mf,
    _unaweza vp soma shule yenye walimu wakutosha pia,mnajaliwa na kufatiliwa vzr..then unpiga 4..tena peke yk(UZEMBE)
    Xax,
    utamlinganish vp na yle anayesoma shule zsizo na walimu,then akafel…
    *Kpass au kufel_
    n chaguo la m2,jpokuwa mazingir n km sababu mama..
    N kawaida,w2 ksema w2 wanapofel..lkn,kikubwa ni mazingira ya usomaj ya m2 hy n muhimu kuangaliwa…
    _KAMA UZEMBE,
    TUSEME…

  6. omar

    daa bola ulivyowachana watu namna hiyo yaani wanaboa kichizi,huyo ni mwanafunzi kama wanafunzi wengine,hiyo ni haki yake aliopata,cha muhimu wabongo tubadilike tusifurahie kufali kwa wenzetu katika kila kitu

  7. Anonymous

    je kam yeye kafel anakusaidia nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>